Home Uncategorized NYOTA WAWILI WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA KESHO, ISHU YA KANGWA IPO...

NYOTA WAWILI WA AZAM FC KUIKOSA SIMBA KESHO, ISHU YA KANGWA IPO NAMNA HI


KESHO Uwanja wa Taifa hapatoshi, ambapo Simba itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa ngao ya Jamii.

Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 23.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kikosi kipo kamili gado kuwavaa wapinzani wao kesho ila kitawakosa nyota wao wawili tu.

“Bruce Kangwa yupo kamili gadoo kuwavaa Simba hivyo ni kazi ya mwalimu tu kumpanga, wachezaji ambao tutawakosa ni Agrey Moris pamoja na Mudathir Yahya,” amesema.

SOMA NA HII  ANTOINE GRIEZMANN AINGIA KWENYE REKODI YA WACHEZAJI GHALI