Home Uncategorized SAMATTA AFUNGUA AKAUNTI MPYA YA MABAO UBELGIJI

SAMATTA AFUNGUA AKAUNTI MPYA YA MABAO UBELGIJI


LICHA ya timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1 na timu ya Kv Muchelen bado Mbwana Samatta alicheka na nyavu.

Samatta alipachika bao la kufuta machozi dakika ya 45 ambalo lilidumu mpaka mwisho wa dakika 90 na timu yake kupoteza pointi tatu muhimu.

Huu unakuwa mchezo wa pili kwa Samatta kucheza na anafungua akaunti na bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Msimu uliopita Samatta alipachika jumla ya mabao 23 na timu yake ilitwaa ubingwa

SOMA NA HII  MWANA FA:NIMEPONA CORONA, WADUDU WALINING'ANG'ANIA