Home Uncategorized SIMBA KUPOKEA TUZO CAF

SIMBA KUPOKEA TUZO CAF


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Ofisa Habari wake Haji Manara, umesema kuwa unaweza kupata tuzo kutoka CAF ya kujaza Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam msimu huu.


Manara ameeleza kuwa msimu uliopita Simba ndiyo iliingia watazamaji wengi kuliko timu zote Africa na mwaka huu wamedhamiria kuendelea kujaza uwanja.

Amefunguka kuwa Simba imekuwa na mashabiki wengi wanaoenda kutazama mechi zake na pengine kwa msimu huu dalili ya kupata tuzo inaweza kuwaangukia wao.

“Sisi ndiyo timu pekee tuliojaza uwanja kuliko timu zote Afrika msimu uliopita tukiwazidi hadi waarabu.

“Nadhani msimu huu CAF wanaweza wakatoa tuzo maalum kwetu kwasababu tumejipanga vizuri zaidi.”
SOMA NA HII  VPL:MWADUI 0-1 YANGA