Home Uncategorized SIMBA: TUPO FITI KUMENYANA NA POWER DYNAMO

SIMBA: TUPO FITI KUMENYANA NA POWER DYNAMO

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuelekea kwenye SportPesa Simba Wiki wamejipanga kufanya makubwa msimu ujao na wataanza kufanya hivyo kesho kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo.

Simba kesho itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki kwenye kilele cha SportPesa Simba wiki utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Patrick Ausssems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kirafiki kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.

“Tumefanya maandalizi mazuri nchini Afrika Kusini na tupo sawa kwa ajili ya ushindani wa kimataifa na kitaifa hivyo tuna amini tutafanya vizuri kwani muda upo na uwezo tunao,” amesema.
SOMA NA HII  RATIBA YA LEO OKTOBA 20 NDANI YA LIGI KUU BARA