Home Uncategorized SIMBA YAWAANGUKIA MASHABIKI WAKE

SIMBA YAWAANGUKIA MASHABIKI WAKE


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna neno la kusema kwa sasa kwa mashabiki wake zaidi ya kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi jana uwanja wa Taifa.

Simba jana ilicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Power Dynamo na iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huo ambao ulivuta hisia za mashabiki wengi ulikuwa na ushindani na kila timu ilipambana kutafuta matokeo chanya.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuna jambo jngine la kuwaambia mashabiki na wapenzi wa Simba zaidi ya shukrani.

“Mengi makubwa ambayo mmefanya kwa kuitikia wito hakuna cha kuwaambia zaidi ya kusema asante kwa sapoti yenu na kujitokeza kwenu uwanja wa Taifa.

“Picha linaanza siku yenyewe ilikuwa ni katikati ya wiki sipati picha kama ingekuwa siku ya mapumziko namna ambavyo wana Simba wangeitikia ila yote kwa yote asanteni sana,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA WAIPIGA KIJEMBE SIMBA KISA VIKAO VYA USIKU.... KAMWE AFUNGUKA HAYA