Home Uncategorized YANGA YAINGIA ANGA ZA SIMBA ISHU YA MAVAZI

YANGA YAINGIA ANGA ZA SIMBA ISHU YA MAVAZI


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kama Kocha Mkuu wa  Simba ataamua kuendelea kuvaa mavazi meupe hawezi kumshangaa kwani ni maamuzi yake.

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba anapenda kuvaa mavazi meupe akiamini kwamba yanabeba bahati ya ushindi hata jana pia uwanja wa Taifa alitupia mavazi hayo na timu yake ikashinda mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamo.

Zahera amesema kuwa:- “Kwa upande wa mavazi kama yeye anapenda kuvaa mavazi meupe akiamini yana bahati hilo ni juu yake kwani kila mtu ana maamuzi yake.

“kwa sasa nami nina maamuzi yangu kama msimu uliopita nilikuwa nina mavazi yangu ambayo yalikuwa yananitofautisha na wengine, kama ilivyo upande wa magari ninaweza kutumia Mercedes Benz na asinipangie mtu,” amesema.

SOMA NA HII  NENO LA KAGERA SUGAR KWA WATANZANIA WOTE KUHUSU CORONA