Home Uncategorized WALIOOA FC VS WASIOOA KESHO HAPATOSHI UWANJA WA CHUO CHA USTAWI DAR

WALIOOA FC VS WASIOOA KESHO HAPATOSHI UWANJA WA CHUO CHA USTAWI DAR


Hatimaye ule mpambano wa kukata na shoka kutoka katika Kampuni ya Global Group, kati ya timu ya Waliooa FC dhidi ya vijana Wasiooa unapigwa kesho katika Uwanja wa Chuo cha Ustawi jijini Dar.

Timu ya Waliooa FC chini ya kocha mwandamizi Elvian Stambuli ‘Ferguson’ wameweka kambi kwenye Hotel ya Autriums jijini Dar es Salaam, huku timu ya Wasiooa wakiwa wameweka katika Hoteli ya Wanyama.

Aidha nahodha wa kikosi cha Waliooa FC, Philip Nkini ametambulisha wataoanza siku hiyo kuwa ni mastaa wake tegemeo, Eric Shigongo atavaa jezi namba kumi, Abdallah Mrisho jezi namba nane, huku Saleh Ally akivaa jezi namba 14 na Samson Mfalila jezi namba 12.

Kwa upande wa timu ya Wasiooa FC waliopo chini ya udhamini wa Kessy Marketing Aggency, wataongozwa na nahodha Omary Mdose ‘Luiz’, Marco Mzumbe ‘Alonso’, Abdulghafal Ally ‘Messi’, Ayoub Dotto ‘Neymar’, Said Ally ‘Fonte’ na Issa Liponda ‘Nuno Santo’.

SOMA NA HII  COASTAL UNION:BADO TUTAZIDI KUPAMBANA, KESHO WANA KIBARUA MBELE YA KAGERA SUGAR