Home Uncategorized KARIA AZIDI KUWAUMIZA ZAIDI YANGA NA ZAHERA, AJA NA KAULI YA KUTISHA

KARIA AZIDI KUWAUMIZA ZAIDI YANGA NA ZAHERA, AJA NA KAULI YA KUTISHA


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa halitakuwa na huruma kwa klabu yoyote itakayotaka kubadili rangi ya nembo ya wadhamini wao kwa msimu huu wa 2019/20 katika Ligi Kuu Bara.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Rais wa TFF kupitia Rais wake, Wallace Karia, kuingia mkataba mwingine wa udhamini na benki ya KCB.

Karia amesema hivyo akieleza wadhamini wanapaswa kuheshimiwa hivyo haitaruhusiwa timu yoyote ile kuvaa jezi ambazo hazina nembo yenye rangi rasmi ya mdhamini.

Aidha, Karia amesema kuwa kwa baadhi ya makocha wanaoingia uwanjani na jezi zenye nembo ya makampuni mengine tofauti na za wadhamini wanaotambulika na TFF lazima wawachukulie hatua.

Kauli hii inakuwa inazidi kuleta wakati mgumu kwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye amekuwa akivaa tisheti zenye nembo ya POLO sambamba na klabu yake ambayo inaelezwa imegomea kuvaa jezi zenye nembo nyekudu kutoka Vodacom.

SOMA NA HII  MATOKEO YA MECHI ZA LEO JUNI 27 VPL