Home Uncategorized KAZI NDO KWANZA IMEANZA, CHIRWA AWA MTAMU KABLA YA KUWAVAA WAZIMBABWE

KAZI NDO KWANZA IMEANZA, CHIRWA AWA MTAMU KABLA YA KUWAVAA WAZIMBABWE


OBREY Chirwaa ameanza kuwa mtamu ndani ya Azam FC baada ya jana kufanya maajabu yake kwa kufunga ‘hattrick’ kwenye mchezo wa kirafiki.

Azam FC ambayo inajiaanda na mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Triangel United ya Zimbabwe Septemba 15 kwa sasa imecheza jumla ya michezo mitatu ya kirafiki.

Kwenye michezo miwili ambayo walicheza dhidi ya Transit Camp ambapo walishinda mabao 3-1, Friends Rangers ambao walishinda mabao 3-0, Chirwa hakufunga hata bao moja na ameibuka jana kwa kufunga mabao matatu wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Pan Africans mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi.

Safu ya ulinzi ya Azam FC inayosimamiwa na Nicholaus Wadada imeruhusu jumla ya mabao mawili huku safu ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao 10.

Idd Cheche , Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa ni mwendelezo wa kufuta makosa ya safu ya ushambuliaji ambayo yamekuwa pasua kichwa ndani ya kikosi.

SOMA NA HII  STARS: TUNAKWENDA KUFANYA KWELI AFCON