Home Uncategorized NGUVU YA SALEH JEMBE YAONEKANA, USHINDI WA MABAO 2-1 WAACHA HISTORIA

NGUVU YA SALEH JEMBE YAONEKANA, USHINDI WA MABAO 2-1 WAACHA HISTORIA


PAMBANO la kukata na shoka kati ya timu ya Waliooa FC dhidi ya Wasiooa FC zote za Makampuni ya Global Group,  jana Ijumaa, lilimaliza ubishi katika Uwanja wa CCM, Sinza, Waliooa FC wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Waliooa FC wakiwa chini ya udhamini mkubwa wa Saleh Jembe blog walikaziwa mwanzo mwisho na wasiooa ila mwisho wa siku wakashinda kwa mbinde na nguvu ya mdhamini Jembe ikaonekana.

Kamati ya ufundi kwa waliooa ikiwa chini ya Mkurugenzi Mtendaji wao, Eric Shigongo  iliandika bao la kwanza kupitia kwa Hamisi Hamsi bao ambalo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili kilikuwa vilevile, Waliooa FC walifanya mabadiliko wakimtoa Mbrazil, Santosh, Amran Kaima na Saleh Ally na nafasi zao kuchukuliwa na Ally Mbetu, Borry Mbaraka na Deo, mabadiliko ambayo yaliiongezea nguvu mpya timu hiyo.

Dakika ya 65, Waliooa  walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Wilbert Molandi ‘Momo’ baada ya kutokea piga-nikupige iliyosababishwa na mpira wa adhabu langoni mwa Wasiooa FC na kujihakikishia ushindi huo.

Dakika ya 84 walifanikiwa kupata mpira wa adhabu baada ya mchezaji wao Abdul kufanyiwa madhambi nje ya 18 ndipo bao la kideo likafungwa na Saidy Ally.

SOMA NA HII  VIDEO MPYA: DIAMOND PLATNUMZ – KANYAGA