KLABU ya Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wake, Hassan Bumbuli imekiri kuwa taratibu haziwaruhusu wachezaji kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu masuala ya ndani ya Klabu na mambo wanayokutana nayo kama sakata la kipa wao, Ramadhani Kabwili.
Kabwili alisema; “Simba waliwahi kunifuata kipindi tupo na kocha Zahera, nilikuwa na kadi mbili za njano na kwenye mchezo wa Yanga na JKT Tanzania, walitaka nitafute kadi ya njano makusudi ili wanipe gari ya IST mpya na nikose mchezo ujao wa watani,” Ramadhan Kabwili.
Ofisa Habari wake, Hassan Bumbuli amesema; “Sisi kama Yanga tutakaa na Kabwili kuzungumza nae kwa undani, Kabwili ni Mchezaji wa Yanga hivyo tutampa ushirikiano wa kutosha katika hili baada ya kumsikiliza.
“Ni kweli wachezaji hawaruhusiwi kuongea na vyombo vya habari lakini kwa kuwa imetokea na Kabwili ni mchezaji wetu hayo mambo ni ya ndani ya klabu, lakini kuhusu hizo tuhuma tutashirikiana nae kuona mambo kama haya yanakoma kama ni kweli yapo.
“Niwaombe wadau wenye ushahidi pia wajitokeze sio katika hili tu, hata vitendo vingine kama hivi ili tukomeshe mambo kama haya kwenye mpira wetu,” amesema Bumbuli.