Home Uncategorized HIKI NDICHO KIWANGO CHA MISHAHARA KWA WACHEZAJI SIMBA, NI BALAA ZITO

HIKI NDICHO KIWANGO CHA MISHAHARA KWA WACHEZAJI SIMBA, NI BALAA ZITO


Imefahamika kuwa, kiwango cha mishahara ya wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi la Simba ni Sh Mil 350 ambapo kwa mwaka inakadiriwa kufi kia Sh Bil 4.

Hilo limebainika siku chache baada ya mwekezaji wa klabu hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kusema kwa mwaka Simba inalipa wachezaji mishahara kufi kia Sh Bil 4.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mishahara hiyo ni kwa wachezaji 28 na viongozi wa benchi lote la ufundi.

Mtoa taarifa huyo alisema kiasi hicho cha fedha kimewazidi watani wao Yanga ambao wenyewe mishahara yao kila mwezi inagharimu Sh Mil 120 pekee ikijumuisha wachezaji 28.

“Maswali mengi yaliibuka mara baada ya Mo kutangaza kiwango cha mishahara anayolipa kufi kia Sh Bil 4, mashabiki wa Simba wana haki ya kuhoji katika hilo. “Ukweli ni kwamba mishahara ya kila mwezi inagharimu Sh Mil 350,” alisema mtoa taarifa huyo.
SOMA NA HII  ISHU YA MORRISON YAVUTA HISIA ZA MASHABIKI WENGI

1 COMMENT