Home Uncategorized HUU NDIO ‘UGONJWA’ WA BEKI KISIKI WA SIMBA

HUU NDIO ‘UGONJWA’ WA BEKI KISIKI WA SIMBA

BEKI kisiki ndani ya kikosi cha Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast amesema kuwa ‘ugonjwa’ wake mkubwa kwenye chakula ni wali samaki.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa mbali na ukarimu wa watu wa Bongo kuna vyakula vingi vizuri anavyovipenda kuvipata wakati wa mlo wake.

“Kwa upande wangu napenda msosi mzuri na kwa hapa Bongo kuna vyakula vingi ila napendelea sana wali samaki, hapo ndipo naona burudani nikipata, iwe ni samaki mchemsho hata wakavu pia ni freshi,” amesema. 
SOMA NA HII  AZAM FC: BADO HATUJAJUA HATMA YA LIGI ITAKUAJE