Home Uncategorized MAZITO AYAFIKIRIA MBELGIJI WA YANGA KWA SASA, AINGIA VITANI NA SIMBA JUMLA

MAZITO AYAFIKIRIA MBELGIJI WA YANGA KWA SASA, AINGIA VITANI NA SIMBA JUMLA


KOCHA Mkuu wa Yanga, LUC Eymael, raia wa Ubelgiji ambaye kwa sasa anamalizia hatua za awali za mkataba wake kabla ya kupewa majukumu rasmi amesema kuwa atafanya mambo makubwa ndani ya klabu hiyo.

Eymael anatarajiwa kutwaa mikoba ya Mwinyi Zahera ambaye alitimuliwa ndani ya klabu hiyo kutokana na kuboronga kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mechi za awali za ligi.

“Natambua kwamba aina ya timu niliyopewa ni ya aina gani, kila kitu kipo wazi kwani wachezaji nimewaona na nilikuwa ninawafuatilia sina mashaka katika hilo na maleng mkakubwa ni kuona timu inapata matokeo.

“Miongoni wa timu ambazo zinatajwa ndani ya Afrika ni Yanga kutokana na ukubwa wake sina wasiwasi, nina amini tutaanza na kuupigania ubingwa kwani ligi bado inaendela na hili linawekezana,” amesema.


Mkataba wa Eymael unatajwa kuwa na vipengele vingi vigumu ambapo mojawapo ni kuhusu kurudisha ari na uwezo wa wachezaji pamoja na suala la kutwaa kombe la ligi ambalo lipo mkononi mwa Simba jambo linaloongeza vita ya moja kwa moja na wapnzani wao wakubwa Simba.

SOMA NA HII  AZAM FC SI YA MCHEZO, ILICHOFANYA JANUARI NI SHIDA TUPU