Home Uncategorized AZAM FC SI YA MCHEZO, ILICHOFANYA JANUARI NI SHIDA TUPU

AZAM FC SI YA MCHEZO, ILICHOFANYA JANUARI NI SHIDA TUPU


AZAM FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba, mwezi Januari,2020 imeweka rekodi ya kucheza mechi tano bila kupoteza mchezo .

Kwenye mechi tano ilizocheza sawa na dakika 450 haijaruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu huku ikilazimisha sare moja pekee.

Imeshinda jumla ya mechi nne ilizocheza na  mwezi Februari ilianza kwa kutoshana nguvu na Mbeya City kwa kufungana bao 1-1, Uwanja wa Samora.

Kesho Jumatano, Februari,5 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons ambayo ilishinda mchezo wake wa kwanza mwezi Februari mbele ya KMC kwa bao 1-0.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA