Home Uncategorized YANGA YAJIPIGIA SINGIDA UNITED 3-1, EYMAEL ACHEKELEA USHINDI

YANGA YAJIPIGIA SINGIDA UNITED 3-1, EYMAEL ACHEKELEA USHINDI

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga leo amesepa na pointi tatu muhimu kwa mara ya kwanza kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Singida United.

Mabao ya Yanga yalipachikwa na Molinga dakika ya 12 na kuwapeleka Yanga mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja na kipindi cha pili waliongeza juhudi na kufunga bao la kwanza kupitia kwa Haruna Niyonzima dakika ya 57 akimalizia pasi ya Morison.

Bao la tatu kwa Yanga lilipachikwa na Yikpe dakika ya 77 baada ya mabeki wa Singida United kujichanganya kuokoa mpira ndani ya 18.

Singida United ilipata bao la ushindi kupitia kwa Six Mwakasege dakika ya 82 akimalizia pasi ya Athuma Chuji.

Kocha Mkuu wa Singida United, Ramadhan Nswanzurimo amesema kuwa wameshindwa kupata ushindi kwa uzembe wao na Eymael amesema kuwa walijipanga kupata ushindi.

SOMA NA HII  KUMBE, CHILUNDA KOCHA ALIMKATAA MOROCCO