UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuelekea Machi 8 hautakuwa na maneno mengi zaidi ya kuwataka mashabiki wakutane uwanjani kuongea kwa vitendo.
Machi 8 kutakuwa na pambano la watani wa jadi litakalowakutanisha Yanga na Simba ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Simba inakumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 kwenye pambano la kwanza lililopigwa Januari 4 Uwanja wa Taifa.
Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:-“Tunaziba kabisa mdomo kuhusu hiyo Machi nane, hapana kikubwa zaidi ya kusema tukutane uwanjani,”.






