Home Uncategorized BARCELONA, REAL MADRID JINO KWA JINO KWA TRAORE

BARCELONA, REAL MADRID JINO KWA JINO KWA TRAORE



KLABU ya Barcelona ipo kwenye mchakato wa kuinasa saini ya nyota wa Wolves, Adama Traore, ambaye alitua kikosini hapo mwaka 2013 akitokea timu ya Barcelona B.
Inaelezwa kuwa Barcelona wanataka kumrejesha mshambuliaji huyo baada ya kuskia kwamba Real Madrid ni miongoni mwa timu inayotaka kuipata saini ya nyota huyo.
Nyota huyo kwa sasa yupo chini ya Nuno Espirito Santo amekuwa na maendeleo mazuri kwenye mechi zake anazocheza kwenye Ligi Kuu England.
Traore anaamini kwamba akirejea kwenye La Liga atamudu mchezo kutokana na uwezo alionao akiwa ndani ya uwanja na timu anayoipenda ni Barcelona.
“Bado nina mkataba ndani ya timu yangu kwa sasa mpaka 2023 ila ikija Barcelona ama Real Madrid nina amini ni suala la kuketi na kuzungumza,” .
Nyota huyo ametupia jumla ya mabao matano na pasi za mabao 10 akiwa chini ya Nuno.
SOMA NA HII  WAWILI WA SIMBA KUIKOSA COASTAL UNION LEO