Home Uncategorized HIVI NDIVYO ABAROLA WA AZAM ALIVYOWANYIMA POINTI WAPINZANI WAKE KWA KUOKOA PENALTI

HIVI NDIVYO ABAROLA WA AZAM ALIVYOWANYIMA POINTI WAPINZANI WAKE KWA KUOKOA PENALTI


RAZACK Abarola, mlinda mlango namba moja wa Azam FC ameweka rekodi ya kuwatisha wapiga penalti wawili kushindwa kumtungua akiwa langoni na kuipa pointi sita kwenye mechi mbili.
Penalti ya kwanza kwa Abarola kukaa langoni ilikuwa mbele ya Mwadui FC, Januari 27, Uwanja wa Kambarage mwamuzi wa kati alitafsiri kwamba beki Yakubu Mohamed ameunawa mpira ndani ya eneo la 18 na kutoa penalti.
Mshambuliaji Gerald Mdamu alikosa utulivu baada ya kutishwa mbele ya Abarola na kupaisha mpira huo dakika ya sita na Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ilishinda mchezo huo kwa bao 1-0 lililofungwa na Shaban Chilunda dakika ya 20.
Penalti ya pili ilikuwa Februari 11, Uwanja wa Uhuru wakati Azam FC ikishinda kwa bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania ambapo mwamuzi alitafsiri kuwa Daniel Amoah ameunawa mpira ndani ya 18 na kuamua penalti dakika ya 7 na ilipigwa na Sixtus Sabilo dakika ya 9 ikapanguliwa na Abarola.
Mchezo huo Azam FC ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Mudhathiri Yahaya dakika ya 48 na kuifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na imecheza mechi 21
SOMA NA HII  ZANA COULIBARY ATAKA KUREJEA BONGO