Home Uncategorized HIVI NDIVYO ARSEANL WALIVYOPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA EVERTON

HIVI NDIVYO ARSEANL WALIVYOPINDUA MEZA KIBABE MBELE YA EVERTON


BAO la mapema walilopata wapinzani wa Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England lililofungwa na Dominic Calvert-Lewin wa Everton dakika ya kwanza mbele ya Arsenal halikuwasaidia kusepa na pointi tatu.

Eddie Nketiah alirudisha makali dakika ya 27 Kwa kufunga bao lililowarudisha mchezoni na Pierre Emerick Aubameyang alipachika bao la pili dakika ya 33 likapinduliwa na Richarlison dakika ya 45+4.

Aubameyang alirejea kambani tena baada ya dakika moja ya kipindi cha pili kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 46 na kuifanya Arsenal ishinde mabao 3-2 na kusepa na pointi tatu jumla.

Arsenal inafikisha pointi 37 ikiwa nafasi ya tisa Everton ipo nafasi ya 11 na pointi 36 zote zimecheza mechi 27.

SOMA NA HII  HUKU UNITED IKIMPIGA MTU 4-0, RASHFORD NA POGBA WACHEZAJI BORA WA MECHI