Home Uncategorized JKT TANZANIA; MECHI YETU DHIDI YA SIMBA NI NGUMU, ILA TUNAZITAKA POINTI...

JKT TANZANIA; MECHI YETU DHIDI YA SIMBA NI NGUMU, ILA TUNAZITAKA POINTI TATU

ABDALLAH Mohamed ‘Bares’, Kocha mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa mchezo wa kesho mbele ya Simba ni mgumu ila kikosi kipo tayari kupata ushindi.

JKT Tanzania itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-1 na Simba kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa wachezaji wapo tayari kupata matokeo mazuri mbele ya Simba.

“Ni mchezo mgumu kwetu hilo lipo wazi ila halitukatishi tamaa kwamba hatuwezi hapana, tupo tayari na tumejipanga kuona namna gani tushinda mbele ya Simba na kuzipata pointi tatu.

“Morali ya wachezaji ni kubwa na kila kitu kipo sawa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani,” amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA YANGA KUSHUSHA PANCHA MOJA MATATA UONGOZI WAFUNGUKA, WAKIRI KUWAFUATILIA KWA UKARIBU