Home Uncategorized NDINGA MPYA KABISA KWA MIA NANE TU AMA JERO, NI RAHISI FANYA...

NDINGA MPYA KABISA KWA MIA NANE TU AMA JERO, NI RAHISI FANYA HIVI


BAHATI nasibu ya Jishindie Gari Mpya iliyoanzishwa na Kampuni ya Global Publishers kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra, imezinduliwa rasmi jana Alhamisi, Februari 27, 2020.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akimwakilisha rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia.

Bahati nasibu hiyo iliyozinduliwa rasmi jana Alhamisi katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori jijini Dar, mshindi mmoja ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo mpya kabisa.

Mbali na mshindi kuondoka na gari, pia kuna zawadi zingine zitakazotoka kila wiki ambazo ni simu za mkononi aina ya Smati Kitochi.

JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi (Tsh 800) au Spoti Xtra (Tsh 500), kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.


JINSI YA KUTUMA:


Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.


Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

SOMA NA HII  COASTAL UNION: TUMEADHIBIWA KWA MAKOSA YETU WENYEWE