Home Uncategorized SINGIDA UNITED HUKO MAMBO BADO

SINGIDA UNITED HUKO MAMBO BADO


SINGIDA United imeanza kwa kuangukia pua tena mzunguko wa pili kwa kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Mwadui FC ya Shinyanga.
Sare hiyo inaifanya Singida United kubaki nafasi ya 20 kwenye msimamo ikiwa na pointi 11, imeshinda mechi mbili pekee na kupoteza mechi 13 na imeambulia sare tano.
Akizungumza na Saleh Jembe, Cales Katemana, Ofisa Habari wa Singida United alisema kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa jambo linalowafanya washindwe kupenya ila watapambana kutoka kwenye wakati huu mgumu.
“Kwa sasa mambo kwetu bado magumu kwani matokeo ambayo tunayapata sio yale ambayo tunayatarajia, matumaini yetu ni kwamba muda wa haya yote utakwisha na tutarejea kwenye furaha upya mashabiki watupe sapoti,” alisema Katemana.

SOMA NA HII  YANGA LEO TUNAMALIZANA MAHESABU MAPEMA KWA TOWNSHIP ROLLERS