Home Uncategorized YANGA :HAKUKUWA NA NAMNA GWAMBINA ILIKUWA LAZIMA ICHAPWE TU

YANGA :HAKUKUWA NA NAMNA GWAMBINA ILIKUWA LAZIMA ICHAPWE TU


HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hakukuwa na namna ilikuwa lazima Gwambina FC ifungwe ili kurejesha furaha kwa mashabiki na nguvu kwa wachezaji.

Yanga ilishinda bao 1-0 mbele ya Gwambina FC, jana Februari 26 Uwanja wa Uhuru kweye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora na kutinga hatua ya robo fainali.

Niyonzima amesema:” Tulikuwa hatuna chaguo la kufanya licha ya wapinzani wetu kupambana kutafuta matokeo nasi tulikuwa tunahitaji matokeo kwani hatukuwa na chaguo lingine zaidi ya kupata ushindi ukizingatia kwamba tumetoka kupata sare nne mfululizo.” amesema.

Bao hilo la ushindi alifunga Niyonzima dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 lilidumu mpaka mwisho wa kipyenga.

SOMA NA HII  SIMBA KUANZA HESABU ZA KUFUKUZIA UBINGWA MEI 27