SIMBA leo imemalizana na Azam FC kwa ushindi wa mabao 3-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ilianza kuzifumua nyavu za Aishi Manula dakika ya 4 kupitia kwa Nevere Tegere na iliwachukua dakika nne Simba kurekebisha makosa yao kupitia kwa Erasto Nyoni.
Dakika ya 14 Deo Kanda aliongeza msumari wa pili na kuifanya Azam FC kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao moja huku Simba ikiongoza.
Kipindi cha pili Azam FC walikuja kwa kasi na kuweka mzani sawa dakika ya 49 kupitia kwa Idd Seleman ‘Naldo’ na kufanya ngoma iwe 2-2.
Meddie Kagere alikuja kuweka usawa kwa Simba ambapo alifunga bao la ushindi dakika ya 72 ambalo lilipa pointi tatu Simba.
Obrey Chirwa dakika ya 83 alipachika bao matata baada ya Manula kutema shuti la Richard Djod ila mwamuzi alitafsiri kuwa aliotea.
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe jumla ya pointi 68 kibindoni ikiwa nafasi ya kwanza na Azam FC inabaki na pointi 48 zote zikiwa zimecheza mechi 26.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.