TIMU ya Namungo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imekuwa ni moto wa kutokea mbali kwa timu ambazo zimepanda daraja msimu huu.
Kocha Mkuu wa timu hiyo ni Hitimana Thiety ambaye falsafa yake kubwa ni kuwategemea vijana na anaawaamini wengi kwa kuwapa majukumu makubwa.
Kwa sasa timu yake ikiwa inashika nafasi ya nne baada ya kucheza mech 25 na kujikusanyia pointi 47.
Namungo pia imekuwa timu pekee ambayo kinara wa kutupia mabao kwao ni mzawa na anatengeneza pasi za mwisho.
Reliats Lusajo kwa sasa ametupia mabao 10 akiwa na pasi za mwisho tatu hii inaonyesha namna gani vijana wakiaminiwa wanaweza.
Kuwa nafasi ya nne na kufikisha pointi 47 kwenye ligi kwa timu iliyopanda daraja sio kitu chepesi lakini kinachotakiwa kujiuliza inawezaje kulinda thamani yake.
Kikubwa kwa sasa uongozi wa Namungo unapaswa ujifunze kulinda hadhi yao na kuachana namasuala ya siasa.
Yasije kutokea kama ilivyokuwa kwa Mbeya City ile iliyopanda daraja kwa kasi na kutikisa ufalme wa Yanga na Simba mwisho wa siku kwa sasa inahaha kujinusuru kushuka daraja.
Ukiachana na Mbeya City kuna timu inaitwa Singida United ilikuja kwa moto mpaka inamaliza ligi msimu wake wa kwanza ikiwa nafasi ya nne kwa sasa mambo bado.
Kila la kheri Namungo mnastahili pongezi lakini mnapaswa mjipange upya msianguke.
Home Uncategorized SPIDI YA NAMUNGO INASTAHILI PONGEZI LAKINI KAMA KUNA MCHANGANYO WA SIASA ANGUKO...