MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar uliokuwa leo majira ya saa 10:00 umeahirishwa hadi kesho saa 3:00 asubuhi.
Mchezo huo umeahirishwa kutokana na mvua iliyonyesha muda mfupi kabla ya mchezo kuanza uwanja wa Ushirika Mosi ambao umejaa maji.