Home Uncategorized ALIYEMCHEZEA RAFU FEI TOTO ARUDI KWA MASHABIKI KUOMBA MSAMAHA

ALIYEMCHEZEA RAFU FEI TOTO ARUDI KWA MASHABIKI KUOMBA MSAMAHA


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amesema kuwa anawaomba radhi mashabiki kwa kitendo chake cha kumchezea mchezo usio wa kiungwana kiungo wa timu ya Yanga, Fei Toto.

Wakati Simba ikichapwa bao 1-0 na Yanga, Chama alimchezea rafu Fei Toto ambayo mwamuzi hakuiona ispokuwa kamera za Azam TV zilinasa tukio hilo.

Chama amesema kuwa amemalizana na Fei Toto kwa kuwa alimuomba msamaha baada ya kumaliza mchezo huo na kuelewana hivyo anaomba msamaha kwa mashabiki.

“Najua nilifanya kitendo kisicho cha kiuungwana ila ilikuwa ni kitendo ambacho sikutarajia, nimemuomba msamaha Fei Toto na kwa sasa ninawaomba radhi mashabiki,”.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR