Home Uncategorized AZAM V SIMBA NI VITA YA KIBABE HAYA HAPA KUONGEZA UTAMU WA...

AZAM V SIMBA NI VITA YA KIBABE HAYA HAPA KUONGEZA UTAMU WA VITA TAIFA


UWANJA wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku leo kutakuwa na kazi ya vigogo wa Lgi Kuu Bara kumenyana kuzisaka pointi tatu muhimu.
Azam FC itakuwa nyumbani kuikaribisha Simba kwenye mchezo wao wa pili wa mzunguko wa pili wa ligi.
Azam FC imetoka kumalizana na JKT Tanzania, mkoani Dodoma, kwenye Uwanja wa Jamhuri na iliambulia ushindi mwembamba wa bao 1-0. Itakutana a Simba iliyotoka kumalizana na KMC kwa ushindi w mabao 2-0 Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo itakuwa imeshika picha ya bingwa ajaye kutokana na ushindani ulipo kwenye ligi kuu bara kutokana na haya yafuatayo:-
Kupunguza na kuongeza ‘gap’ la pointi
Azam FC  ina pointi 48 kibindoni huku Simba nayo ikiwa na pointi 65 tofuti ya pointi 17. Ili Azam FC ipunguze  ‘gap’ la pointi ni lazima iichape Simba mchezo wa leo huku Simba wao wakihitaji kuongeza pointi tatu ili kujitengenezea ufalme wao wenyewe nafasi ya kwanza.
Vita ya tuzo ya Kocha Bora
Kwa mwezi Februari inaonekana wote wmechemka kwani walipokea vichapo na kuwafanya wazidiwe kete na baadhi ya timu nyingine ambazo bado zinapambana. Arstica Cioaba mwenye tuzo ya Kocha bora wa mwezi Januari anahaha kuona anapata ya mwezi Machi baada ya mwezi Februari kutibua mipango yake .
Sven Vandenbroeck, hana bahati kabisa na tuzo ya mchezaji bora kutokana na kupishana nazo hivyo akifanya vizuri mwezi Machi atajisogenza kwenye kiti cha ufalme wa tuzo za makocha.
Mmoja kisasi mwingine rekodi
Azam FC inakumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kufungwa bao 1-0 lililofunwa na Meddie Kagere jambo linalowafanya wapambane kuona namna gani mambo yanakuwa magumu.’WakatI Cioaba anapiga hesab hizo  Sven yeye anawaza rekodi mpya ndani ya ligi kwa kuifunga Azam FC nje ndani.
Vita ya wakali wa pasi za mwisho
Nicolas Wadada, beki wa Azam FC mwenye pasi saba za mabao na  bao moja  atakutana na fundi wa kuwapa pasi za mwisho kwa upande wao Sharaf Shiboub, mwenye pasi sita za mabao na ana bao mija pia mguuni.
Tuzo ya ufungaji bora
Azam FC wao mshambuliaji naba moja ni Obrey Chirwa ambaye ametupia mabao nane kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara  huku Simba wao wakiwa na MeddIE Kagere mwenye mabao 14.
Heshima mtaani
Kwa sasa timu itakayoibuka na ushindi itajiwekea heshima mtaani na kuwafanya mashabiki wapate cha kuongea mbele ya watanni zao kwenye mechi zitakazofuata.
Kila kocha anahitaji kuona anaheshimiwa na wapinzani wao kwa kumpa ichapo cha maana kitakachowafanya wakikutana mchzo wa pili tambo ziishe.

SOMA NA HII  KARIA AZIDI KUWAUMIZA ZAIDI YANGA NA ZAHERA, AJA NA KAULI YA KUTISHA