Home Uncategorized KOCHA MTIBWA SUGAR: TAHADHARI YA CORONA NI LAZIMA IFUATWE NA WATU WOTE

KOCHA MTIBWA SUGAR: TAHADHARI YA CORONA NI LAZIMA IFUATWE NA WATU WOTE


KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa ni lazima kila mmoja achukue tahadhari ya kujikinga na Virusi vya Corona ambavyo kwa sasa ni janga la dunia nzima.

Corona ilianza kusambaa nchini China mwezi Desemba, 2019 ambapo kwa sasa imekuwa ikisambaa kwa kasi dunia nzima na kufanya shughuli nyingi zinazohusu mijumuiko kufungwa ikiwa ni pamoja na sekta ya michezo ambapo kwa Tanzania, Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda wa siku 30 ili kuzuia maambukizi zaidi.

Katwila amesema:”Inapotokea janga la aina hii hakuna haja ya kuleta utani ni lazima kila mmoja kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za afya ili ajilinde yeye pamoja na wengine, kwetu sisi pia tunajali na kufuata utaratibu uliowekwa kwani hakuna namna nyingine ya kufanya kwa sasa,” 

SOMA NA HII  SIMBA WANA MAMBO MATANO YANAYOWAPA NAFASI YA KUIFUNGA PLATEU, LAKINI SIO WEPESI