Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA ATUMIA DAKIKA 1,350 KUSAKA POINTI 26, MECHI MBILI ZA...

MBELGIJI WA YANGA ATUMIA DAKIKA 1,350 KUSAKA POINTI 26, MECHI MBILI ZA MWANZO ILIKUWA KICHAPO


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amekiongoza kikosi chake kwenye mechi 15 za Ligi Kuu Bara sawa na dakika 1,350 baada ya kupokea mikoba ya Mwinyi Zahera aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, ameshinda mechi saba, sare tano na kuchapwa mechi tatu.
Ndani ya dakika 1,350 alishuhudia timu yake ikifungwa mabao 10 huku safu safu yake ya ushambuliaji ikifunga  mabao 15, kwenye pointi 45 alizokuwa akisaka ameambulia pointi 26 na kuziyeyusha pointi 19 kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
Mechi zake mbili za mwanzo aliambulia kichapo mfululizo ilikuwa namna hii:-Januari 15,Yanga 0-3 Kagera Sugar, Januari 18, Azam 1-0 Yanga, mwezi Februari alikomaa na kuibukia kupokea kichapo Machi 12, KMC 1-0 Yanga.
Hizi hapa za ushindi,:-Januari 22, Singida United 1-3 Yanga, Februari 2, Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Februari 5, Yanga 2-1 Lipuli, Februari 8, Ruvu Shooting 0-1 Yanga, Februari 29, Yanga 2-0 AllianceMachi 3, Yanga 2-0 Mbao, Machi 8, Yanga 1-0 Simba.

Sare zake hizi hapa:-Februari 2, Yanga 1-1 Mbeya CityFebruari 15, Yanga 0-0 Prisons, Februari 18, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Februari 23, Coastal Union 0-0 Yanga, Machi 15, Namungo 1-1 Yanga.
SOMA NA HII  MEDDIE KAGERE ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA