Home Uncategorized MKUDE ATOA TAMKO KUHUSU HATMA YAKE NDANI YA TIMU YA TAIFA YA...

MKUDE ATOA TAMKO KUHUSU HATMA YAKE NDANI YA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA

JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya Simba amesema kuwa bado ataendelea kulitumikia Taifa lake la Tanzania iwapo atapewa nafasi ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Inaelezwa kuwa kabla ya kambi ya Taifa Stars kuvunjwa wakati ikijiandaa kwa ajili ya michuano ya CHAN na Afcon, Mkude aligomea kujiunga na kambi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya Corona.

Kocha Mkuu wa Stars, Ettiene Ndayirigaji alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala la Mkude kwa kuwa hajaripoti kambini na hakupata taaarifa zake.

Mkude amesema kuwa:”Bado nipo tayari kuendelea kuitumikia timu yangu ya taifa iwapo nitapata nafasi mambo yaliyotokea awali ni kutokana na matatizo ya kifamilia hivyo nikipata nafasi ya kulitumikia taifa langu nitafanya hivyo,”. 

SOMA NA HII  MORRISON:MPIRA SIO VITA, NILIKUWA YANGA SASA NIPO SIMBA