Home Uncategorized KUMBE FIRMINO ALITABIRIWA MAKUBWA TANGU MDOGO, WAZAZI WAKE WALIMZUIA KUCHEZA SOKA WAKIHOFIA...

KUMBE FIRMINO ALITABIRIWA MAKUBWA TANGU MDOGO, WAZAZI WAKE WALIMZUIA KUCHEZA SOKA WAKIHOFIA ANGEKUJA KUWA KIBAKA



ROBERTO Firmino Barbosa de Oliveira, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Liverpool inaelezwa kuwa wazazi wake walikuwa hawataki kumuona akicheza soka wakihofia kuumia kwa nyota huyo kwani walikuwa hawana uwezo wa kumtibia.

Alizaliwa Oktoba 2,1991 huko Trapiche da Barra, Brazil na alikuwa karibu na Uwanja wa Cacophony ambao una uwezo wa kuchukua watu 20,000 uliopo karibu na Estadio Rei Pele.

Sababu nyingine iliyowafanya wazazi wa nyota huyo kuhofia kumuacha mtoto huyo kutembea mtaani ni kuhofia asije kuwa kibaka tangu akiwa mdogo.

Rafikiye Firmino enzi za utoto, Bruno Barbosa dos Santos amesema :” Ilikuwa ngumu kuwa karibu na Firmino kwani wazazi wake hawakutaka kumuona akijichanganya mtaani na walikuwa wanamlinda kwa ukaribu,”.


Dedeu ambaye naye ni rafiki yake wa utotoni amesema :”Mama yake Roberto alikuwa anahofu na majirani pamoja na marafiki zake huenda wangemfanya mtoto wake kuwa mporaji wa porini,”. 


Guilherme Farias, Kocha wa Firmino enzi za utoto akiwa ndani ya kikosi cha CRB kwa muda wa miaka miwili amesema kuwa ilikuwa ngumu kwa nyota huyo kujiunga na klabu hiyo kwani kuna wakati alikuwa anamuwekea ngazi kwenye ukuta ili awahi mazoezini kutokana na uwezo aliokuwa nao.

“Ana nguvu kubwa na uwezo wa kufanya kazi, alikuwa anapenda kufikia malengo yake na mchezaji aliyekuwa anampenda alikuwa ni Pele, niligundua jambo kwake kutokana na moyo wake wa kujitoa.


“Nilikuwa ninawaambia watu kwamba ataibukia kwenye timu ya Taifa wengi walikuwa wananicheka kwa sasa hakuna anayeongea kwani maneno yangu yametimia nimewanyamazisha mdomo wao,” amesema.

SOMA NA HII  SHIBOUB ATOA TAMKO SIMBA - VIDEO