Home Uncategorized VIONGOZI WA KLABU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUU ENGLAND KUKUTANA LEO, ISHU YA MIKATABA...

VIONGOZI WA KLABU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUU ENGLAND KUKUTANA LEO, ISHU YA MIKATABA NAYO NI SHINIKIZO

IMEELEZWA kuwa nguvu kubwa kwa sasa inayotumika kuimaliza Ligi Kuu ya England kabla ya Juni 30 ni kutokana na kandarasi za wachezaji wengi kukaribia kukamilika.
Ligi Kuu ya England imesimamishwa mpaka Aprili 3 kutokana na kusambaa kwa virusi vya Corona na inaelezwa kuwa iwapo ligi hiyo itafutwa vinara Liverpool wasahau kupewa kombe lao.
Leo viongozi wakubwa wa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu England watakutana kujadili mpango wa kumaliza ligi yao na inatarajiwa kuanza kuendelea Aprili 4.
Imeelezwa kuwa kucheza kabla ya Juni kutaongeza nguvu kwa wachezaji kuendelea kupambana kutokana na mikataba ya wachezaji wengi kukaribia kuisha jambo litakaloongeza ugumu kwao kupambana ndani ya uwanja iwapo mikataba yao itakuwa imekwisha.
SOMA NA HII  MARTIN APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA BARCA