Home Uncategorized LORENZO SANZ, ALIYEKUWA RAIS WA REAL MADRID AFARIKI

LORENZO SANZ, ALIYEKUWA RAIS WA REAL MADRID AFARIKI

Rais wa zamani wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Lorenzo Sanz amefariki dunia kwa virusi vya corona.

 Sanz mwenye umri wa miaka 76 alikuwa Rais wa Madrid kwa miaka mitano (1995 – 2000) alifariki jana wakati akipatiwa matibabu ya virusi vya Corona.

Akiwa madarakani 1998 alifanikisha timu yake ya Madrid kucheza fainali ya kwanza ya michuano ya Ulaya baada ya miaka 32.

 Enzi za uongozi wake akiwa ndani ya Bernabeu timu ya Real Madrid ilishinda Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili.

Mwanae amesema kuwa :”Baba yangu amefariki huu ndio mwisho wake kwa sasa, amekuwa kiongozi mzuri na mtu ambaye nimekuwa nikimfuata katika mengi, alikuwa ni mchapakakazi na ni miongoni mwa watu ambao sijawahi kuwaona,” ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.
,

SOMA NA HII  KESI YA MALINZI NGOMA BADO MBICHI, UAMUZI WA KESI SASA JULAI 23