Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA AWASHANGAA WACHEZAJI WAKE KUPOTEZA MBELE YA KMC

MBELGIJI WA YANGA AWASHANGAA WACHEZAJI WAKE KUPOTEZA MBELE YA KMC


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameshangazwa na wachezaji wake kupoteza mbele ya KMC licha ya kutoka kuimaliza Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopita Machi 8 kabla ya kumenyana na KCM Machi 11.

Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jambo lililomshangaza Mbelgiji huyo.

“Sijajua sababu ya wachezaji wangu kushindwa kupata ushindi mbele ya KMC, mipango ilikuwa sawa na kila mchezaji nilimpa majukumu yake nashangaa wamekwama kuibuka na ushindi ilihali tumetoka kuichapa Simba.

“Bado kuna kazi ya kufanya kwa ajili ya kupata matokeo nitazungumza nao tena ili kujua tatizo lipo wapi kwani haina maana kushinda mbele ya Simba tujisahau na kufikiri tumemaliza kila kitu,” amesema.

Yanga ilifungwa bao hilo dk ya 62 kupitia kwa Salum Aiyee ambaye aliifungia KMC bao lake la kwanza baada ya kujiunga kikosini hapo akitokea Mwadui FC.

SOMA NA HII  MATOLA WA SIMBA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA AZAM FC