Home Uncategorized NYOTA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED AMTABIRIA MAKUBWA SHAW

NYOTA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED AMTABIRIA MAKUBWA SHAW


RIO Ferdinand, beki wa zamani wa Manchester United amesema kuwa kiwango cha nyota Luke Shaw ni cha ajabu akiendelea kupewa nafasi atafanya makubwa ndani ya klabu yake hiyo.

Kwenye mchezo wa Kombe la FA England dhidi ya Derby County, uliochezwa Machi 5, Uwanja wa Pride Park nyota huyo alipachika bao la kuongoza dakika ya 33 huku mabao mengine mawili yakifungwa na Odion Ighalo dk ya 41 na 70.

Ferdinand amesema, nyota huyo anazidi kuwa bora kadri anavyocheza ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri iwapo akipewa nafasi ya kuanza mara Kwa mara.

“Anakuwa imara kwenye uwezo wa nguvu na akili ya kufikiri, anazidi kuwa imara kadri siku zinavyokwenda atawadhihirishia wengi ambao walikuwa wanambeza awali,”.

SOMA NA HII  KIKOSI KAZI CHA KELVIN YONDANI WA YANGA KINA BALAA, WAWILI WA SIMBA NDANI