Home Uncategorized RUVU SHOOTING:TUNAPIGA MPIRA MWINGI KAMA BARCELONA VILE

RUVU SHOOTING:TUNAPIGA MPIRA MWINGI KAMA BARCELONA VILE


 MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa kikosi chao kinapiga mpira mwingi ndani ya uwanja jambo ambalo linawapa matokeo mazuri.


Ruvu Shooting imekuwa kwenye ubora wake ndani ya ligi kwenye mechi zake za hivi karibuni ambapo iliweza kushinda mechi mbili mfululizo baada ya kuanza kuichezesha gwaride Simba kwa kuifunga bao 1-0 kisha iliendelea mwendo wake mbele ya Coastal Union kwa ushindi wa mabao 3-1 zote zilichezwa Uwanja wa Uhuru.


Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa wengi huwa wanaishahau Ruvu Shooting na kuiweka pembeni hawatambui kwamba ni moja ya timu bora zinazotumia wazawa.


“Unajua ndugu yangu wengi wanaiweka kando Ruvu Shooting hawaikumbukikumbuki mpaka pale itakapokuwa labda na mechi na Simba na Yanga lakini sisi nasema tupo na tena tupo imara.


“Wachezaji wetu wote ni wazawa na wanacheza mpira mwingi kama Barcelona na hapa kwa kweli soka linapigwa sio mchezo haya mambo mengine yapo tu lakini soka lipo kweli ujue.


“Kuanzia wachezaji wenyewe mpaka wapishi wote wanalipwa stahiki zao kwa wakati na furaha yetu huku ni kubwa hakuna ambaye hafurahii masisha huku, hivyo bado mambo mazuri yanakuja mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.


Ruvu Shooting ipo nafasi ya 5 ikiwa imecheza mechi 10 ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 ina pointi 16.

SOMA NA HII  BOSI YANGA ATOA TAMKO KUHUSU UHASAMA WA KUHAMA SIMBA