Home Uncategorized PANGA KUSHUKA YANGA KWA MTINDO HUU

PANGA KUSHUKA YANGA KWA MTINDO HUU


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa kuna mpango mkubwa wa kuwapiga chini wachezaji wake wote ambao hawana mchango mkubwa ndani ya timu.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael leo itakuwa uwanjani kumenyana na KMC mchezo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 25.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wanawatazama wachezaji wote wa Yanga kwa wakati ili kujua aina ya wachezaji wenye mchango ndani ya kikosi hicho na wale wasiokuwa na mchango panga linawahusu.

“Tumefanya usajili mkubwa lakini bado kunawachezaji wengine wamekuwa na mchango mdogo kutokana na sababu mbalimbali, kwa sasa tunamaliza tathimini ikikamilika wengine wataaachwa ili kuendelea na maisha mengine,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamepewa madili na Yanga na hawaonekani ndani ya uwanja ni pamoja na David Molinga, Ally Ally, Yikpe Gnamien, Erick Kambamba.

SOMA NA HII  KAZE ANA KAZI YA KUPAMBANA NA VIGONGO VITANO VYA MOTO NOVEMBA