Home Uncategorized POLISI TANZANIA: LIGI KUU BARA SI YA KITOTO

POLISI TANZANIA: LIGI KUU BARA SI YA KITOTO


MARCEL Kaheza, mshambuliajai wa Polisi Tanzania amesema kuwa ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu unawafanya wakomae kusaka matokeo kwenye mechi zao zote ili kujiweka kwnenye nafasi nzuri.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa wamekuwa wakikutana na timu ngumu ambazo zina uzoefu mkubwa ndani ya ligi ila kutokana na maelekezo wanayopata yanawafanya wajiamini wakiwa ndani ya uwanja.

“Kiukweli kwa sasa ligi sio nyepesi ukizingatia kwamba timu nyingi zinashuka daraja, kila mechi kwetu ni fainali tumekubaliana kufanya kazi kwa juhudi na hicho ndicho tunachokifanya tukiwa uwanjani,” amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 42 imecheza mechi 28, mchezo wake uliopita ililazimisha suluhu mbele ya Mtibwa Sugar ikiwa uwanja wake wa nyumbani Ushirika,Moshi.

SOMA NA HII  MIRAJI AINGIA KATIKA REKODI