Home Uncategorized POGBA KUBAKI NDANI YA MANCHESTER UNITED KISA UBORA WA NYOTA WA KIKOSI...

POGBA KUBAKI NDANI YA MANCHESTER UNITED KISA UBORA WA NYOTA WA KIKOSI HICHO



PAUL Pogba, kiungo wa Manchester United kwa sasa imeelezwa kuwa anafikiria kubaki ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya mafanikio yake ya hapo baadaye.
Pogba iliripotiwa kuwa ana mpango wa kusepa ndani ya Old Trafford ili akapate changamoto mpya kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi chake wakati huo ambacho  kinatumia Uwanja wa Old Trafford.
Raia huyo wa Ufarasa kwa sasa imeelezwa kuwa ameridhishwa na kiwango kinachoonyeshwa na timu hiyo na anaamini anaweza kufikia malengo yake iwapo atabaki pamoja na uwepo wa nyota wengi wanaojituma ndani ya kikosi.
Timu ambazo alikuwa anatajwa kuibukia ilikuwa ni pamoja na Juventus ambao walikuwa tayari kuinasa saini yake huku Barcelona na Real Madrid nazo zilitajwa kuingia kwenye vita ya kutaka saini ya nyota huyo ambaye bado hajarejea uwanjani kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Ubora wa Bruno Fernandes aliye chini ya Kocha Mkuu Ole Gunnar Solksjaer umetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazompa furaha nyota huyo mwenye miaka 26 kufikiria kubaki ndani ya kosi hilo.
SOMA NA HII  NAHODHA STARS: WALILAZIMISHA SARE KWETU NASI TUNAKWENDA KUSHINDA KWAO