Home Uncategorized REKODI ZAIBEBA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED

REKODI ZAIBEBA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED

LEO Uwanja wa Taifa Singida United iliyo chini ya Ramadhan Nswazurimo ina kazi ya kutibua rekodi iliyowekwa na Simba pindi wanapokutana kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara tangu kupanda daraja msimu wa 2017/18 kwa kufungwa mechi zote.
Rekodi zinaonyesha kuwa Singida United imekutana na Simba mara tano na imeyeyusha pointi 15 mbele ya Simba na safu yake ya ushambuliaji haijaambulia bao walipokutana.
Kwenye mechi tano Singida United imekubali kufungwa mabao 11 ambapo Simba mechi zote hizo ambazo ni sawa na dakika 450 wametoka bila ngome yao kuguswa.
Matokeo yao ilikuwa namna hii:-2017/18Simba 4-0 Singida United, Uwanja wa Uhuru , Singida 0-1 Simba, Namfua. 2018/19, Simba 3-0 Singida United, TaifaSingida United 0-2 Simba, Namfua. Mchezo wa kwanza msimu huu wa 2019/20, Singida 0-1 Simba, Sheikh Amri Abeid.
Timu zote leo zinakutana zikiwa zimetoka kupokea kichapo kutoka kwa wapinzani wao ambapo Simba imetoka kunyooshwa bao 1-0 mbele ya Yanga na Singida United imetoka kunyooshwa mbele ya Tanzania Prisons mabao 2-1.
SOMA NA HII  NAMUNGO FC: TATIZO LIPO KWENYE MAANDALIZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here