Home Uncategorized SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA KUNYOOSHWA BAO 1-0 NA YANGA

SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA KUNYOOSHWA BAO 1-0 NA YANGA


JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kilichowaponza kushindwa kusepa na pointi tatu jana Machi 8,2020 mbele ya Yanga ni kutokuwa makini kuzitumia nafasi walizotengeneza.

Simba ilichapwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili na kuifanya iache pointi tatu zikisepa jumla kwa Yanga Uwanja wa Taifa.

“Haikuwa kazi nyepesi kwani tulipambana kupata matokeo mambo yakawa magumu kwetu, wapinzani wetu walikuwa vizuri na walitumia nafasi moja waliyoipata tofauti na sisi tulishindwa kuwa makini kuzitumia nafasi tulizozipata.

“Tunajua hali ya mashabiki ilivyo hata sisi pia hatujapenda kupata matokeo haya ila tunawaomba waendelee kutupa sapoti kwani mechi bado zipo nyingi tutafanya vizuri,” amesema.

Simba inabaki kuwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 27 ikiwa na pointi 68 kibindoni huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 50 ikiwa imecheza mechi 25.

SOMA NA HII  YANGA YATAJA SABABU ZA KUSAJILI MSHAMBULIAJI MMOJA