Home Uncategorized UONGOZI WA SIMBA WATAJA SABABU YA KUCHAPWA BAO 1-0 MBELE YA YANGA

UONGOZI WA SIMBA WATAJA SABABU YA KUCHAPWA BAO 1-0 MBELE YA YANGA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kichapo mbele ya Yanga kinawaumiza na wana kila sababu ya kukubali kuchapwa kutokana na makosa yao wenyewe.

Mara ya mwisho Yanga kuibamiza Simba ilikuwa ni mwaka 2016 wakati huo Kocha Mkuu alikuwa Hans Pluijm, raia wa Uholanzi.

Bao la Bernard Morrison limeibuka baada ya miaka minne kumeguka akifunga kwa adhabu ya faulo akiwa nje ya 18 na kumtungua Aishi Manula.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Masingisa amesema kuwa sababu kubwa ya wao kushindwa kupata ushindi mbele ya Yanga ni wachezaji wao kushindwa kujituma ndani ya Uwanja.


 “Kipigo kinaumiza na hasa ukizingatia kwamba tulijipanga kufanya vizuri, hakuna dabi nyepesi hivyo ni vigumu kupata matokeo kiwepesi, ili kushinda ni lazima wachezaji kujitoa kwa dakika 90 kupambana,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YATUA KWA SARPONG, YAIPOTEZA MAZIMA YANGA