Home Uncategorized SURE BOY SASA MAMBO FRESH YANGA WASHINDWE WENYEWE TU

SURE BOY SASA MAMBO FRESH YANGA WASHINDWE WENYEWE TU

ABDULKARIM Amin ‘Popat’ Mtendaji Mkuu wa Azam FC amesema kuwa iwapo Yanga wanahitaji huduma ya mchezaji wao basi wafuate utaratibu.

Kauli hiyo inatoa mwanga kwa mabosi wa Yanga iwapo wanahitaji kuipata saini ya kiungo huyo kazi ni kwao kwani mambo ni fresh labda washindwe wenyewe.

Kwa sasa kumekuwa na taarifa kwamba Yanga wanahitaji huduma ya kuipata saini ya Salum Abubakar,’Sure Boy’ ili akaongeze nguvu ndani ya kikosi chao.

Popat amesema:- “Kama kweli Yanga wanahitaji huduma ya mchezaji wetu Sure Boy ni suala la kukaa mezani na kujadili namna gani tunaweza kujadili.

“Hatuna mashaka na mazungumzo kwani tumefanya hivyo kwa wachezaji wengi ambao walikuwa wanahitajika ikiwa ni pamoja na Ditram Nchimbi ambaye kwa sasa anakipiga Yanga,” amesema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA ASTON VILLA, SAMATTA KUFANYIWA VIPIMO KESHO