MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa maombi yake makubwa ni kuona kwamba Virusi vya Corona vinaiachia dunia iendelee na shughuli zake ili arejee kazini kuendelea kutupia kwenye ligi.
Kagere ndani ya Ligi Kuu Bara kabla ya kusimamishwa alikuwa ametupia mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao kati ya 63 yaliyofungwa na Simba akiwa ni kinara wa kutupia ndani ya ligi.
Kwa sasa Kagere yupo nchini Rwanda akichukua mapumziko ambayo yalitolewa na Serikali baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa Machi 17 kabla ya taarifa nyingine kutolewa Aprili 14 kwamba ligi itaendelea kusimama mpaka pale hali itakapokuwa shwari.
“Ninapenda kuona kwamba hali inakuwa shwari na tunarejea kwenye shughuli zetu za kila siku, ninaamini ikiwa hali itakuwa shwari mambo yataendelea kama kawaida nasi pia tutapata muda wa kuendelea na ligi.
“Ninachokiamini ni kwamba Mungu atatuvusha salama na shughuli zitaendelea kwenye maisha yetu, iwapo itakuwa hivyo basi nitaendelea kutupia kwani ndiyo kazi ambayo ninaipenda,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.