BEKI wa Azam FC, Agrey Moris amesema mazoezi ya kufanya kila mchezaji kivyake si mazuri kuliko yale ya kitimu.
Moris amesema kipindi hiki wachezaji wanafanya mazoezi yao binafsi wanakuwa na wakati mgumu kwani wachezaji walio wengi hawajazoea hali hiyo hivyo ni changamoto kubwa kwao ingawa amesisitiza kuwa wanajitahidi kukubaliana na hali hiyo.
“Huu ni ukweli usiopingika kwani mchezaji anapokuwa na wenzake hata morali zaidi ya kufanya mazoezi inakuwa juu tofauti na akiwa pekee yake ila tunapambana kuhakikisha tunalinda viwango vyetu,” anasema.
Moris amesema yeye amejiwekea programu maalum alizoelekezwa na kocha wake ili kuhakikisha Ligi itakaporejea anakuwa katika kiwango chake kile kile.
Ligi Kuu imesimama zaidi ya siku 30 sasa baada ya Serikali kutangaza kuwepo kwa ugonjwa hatari wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.