Home Uncategorized AZAM, SIMBA NA YANGA ZAKUTANA KWA MFUMANIA NYAVU NAMBA MOJA LIPULI

AZAM, SIMBA NA YANGA ZAKUTANA KWA MFUMANIA NYAVU NAMBA MOJA LIPULI


PAUL Nonga mtupiaji wa Lipuli ameziweka vitani timu tatu kubwa ambazo zinahitaji saini yake kwa sasa ikiwa ni pamoja na Azam FC, Yanga na Simba.
Habari zinaeleza kuwa kwa sasa Nonga amekuwa kwenye hesabu za kuwindwa na timu tatu za juu jambo ambalo limewashtua Lipuli ambao wamemuwahi kwa kumpa mkataba wa awali ili asaini.
“Nonga amebakiza mkataba wa miezi sita ndani ya Lipuli na amekuwa akiwindwa na timu kubwa ambazo ni Yanga, Azam na Simba zote zikihitaji kupata saini yake jambo hilo limewafanya Lipuli wamuwahi kwa kumpa mkataba wa awali,” ilieleza taarifa.
Nonga amesema: “Kwa sasa ni kweli nimebakiza kandarasi ya miezi sita ndani ya Lipuli na nina dili tatu mkononi ikiwa ni pamoja na ya timu yangu, wakati ukifika nitasema nitakuwa wapi.”.

 Nonga ambaye ndani ya Lipuli anavaa kitambaa cha unahodha, ametupia mabao 11 na kutoa pasi nne za mabao.

Chanzo Championi
SOMA NA HII  KOCHA STARS: UWEZO WA WACHEZAJI UNAONGEZEKA KILA SIKU