Home Uncategorized CHOMOKA NA GARI YAZIDI KUNOGA

CHOMOKA NA GARI YAZIDI KUNOGA


MAMBO ni yente kila kona ya nchi kwa lugha ya vijana wa kisasa kufuatia kushika kasi kwa promosheni namba moja kwa sasa Tanzania, nazungumzia bahati nasibu ya chomoka na gari mpya aina ya Toyota FunCargo inayoendeshwa na Magazeti Bora ya michezo, Championi na Spoti Xtra.
Mbali na zawadi hizo, kila wiki washindi 10 wataondoka na simu janja mpya za mkononi aina ya smart kitochi zikiwa zimesheheni bando la bure na App ya Global ambayo ndani yake ina +255 Global Radio na Global TV Online.
JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi au Spoti Xtra, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
JINSI YA KUTUMA
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.
MASHARTI YA KUSHIRIKI
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda.
Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.
SOMA NA HII  SARPONG WA YANGA AWAKIMBIZA NYOTA WOTE WA SIMBA