Home Uncategorized DILI LA KAGERE KUIBUKIA HISPANIA LIMEKAA HIVI

DILI LA KAGERE KUIBUKIA HISPANIA LIMEKAA HIVI


WAKALA wa straika wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amefunguka kwamba dili la straika wake kutakiwa na klabu ya Hispania limekuwepo na kitu pekee ambacho kinakwamisha suala hilo ni mabosi wa mchezaji wake, Simba.
Gakumba ameongezea kuwa alipata dili hilo la Kagere la kutakiwa na moja ya klabu ambazo zinashiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) ambapo walikuwa wanamhitaji straika huyo mwenye mabao 19 kwenye Ligi Kuu Bara.
Wakala huyo amesema kuwa alipata dili hilo baada ya kuzungumza na rafiki yake ambaye anaishi Hispania ambapo alikuwa anataka ampeleke straika huyo kwa ajili ya mkopo ambao angeweza kununuliwa moja kwa moja.
“Rafiki yangu anayekaa Hispania ndiye ambaye aliniambia kuwa moja ya klabu za ligi kuu ya nchi hiyo inamtaka Kagere kwa ajili ya mkopo na kama akifanya vizuri basi angeweza kusajiliwa moja kwa moja.
“Kwa sasa wao wanasubiri majibu kutoka huku ambapo ishu kubwa ni suala la mkataba wake na Simba na wao ndiyo ambao wanashikilia dili hilo.
“Nilizungumza nao na wao kwa sasa wanasikilizia juu ya hilo, ni dili ambalo kama litashindikana litanifanya nikose fedha nyingi,” amesema.

Chanzo: Championi
Licha ya jina la klabu hiyo kufichwa, inaelezwa kuwa ni Levante ndiyo inayomhitaji straika 
SOMA NA HII  VIFAA VIWILI VYASAINI YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here